Monday 4 May 2015

Mavazi ya Maofisini





































Popote pale unapofanyia kazi ndio ofisi yako unapaswa kupapenda na kupaheshimu hasa kimavazi.

Ni vema basi kwa wale wanaofanya kazi maofisini wajue jinsi ya kuvaa wawapo maofisini tofauti na mtoko mwingine.

Mavazi yako uwapo sehemu ya kazi ni muhimu kukuwakilisha sehemu husika ulipo

Ni muhimu na heshima kama ;sememu yako ya kazi utaipa kipaumbele kwa kuvaa mavazi yenye hadhi ya sehemu husika

Saturday 18 April 2015

Jinsi ya kutengeneza kucha zako

















































Kucha zinaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa kuboresha mwonekano wako kama utazijali kuzipenda na kuzitunza vizuri.

Ni jambo la busara na linalopendeza kama ukijitahidi kuweka kucha zako katika hali ya
 usafi kwa kuziosha vizuri na kuzikata katika saizi ya kupendeza.

Kuna baadhi ya watu wanaopenda kufuga kucha zao japo sio salama sana kiafya. Ila kama umependa kufuga kucha zako basi jitahidi kuzifanyia usafi wa hali ya juu ili ziwe na mwonekano wa kuvutia na kupendeza zaidi.

Kucha nzuri na zenye matunzo zinaongeza urembo wako kwa wanawake pia  kwa wanaume zinakufanya uvutie zaidi na kuonekana wa kisasa.


Pia kucha zinaweza kuongeza mvuto zaidi pale zinapopakwa rangi kwa mpangilio mzuri na unaofaa.